Pavard atua Bayern Munich
Klabu ya Bayer Munich imetangaza itamsajili beki Benjamin Pavard kutoka Stuttgart ya huko huko Ujerumani katika majira ya kiangazi mwaka huu.
Mabingwa hao wa Bundesliga wanataraji kumsajili beki huyo,22, wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitano.
.
“ Tunafuraha na fahari kuweza kuinasa huduma ya mchezaji kama yeye “ amesema mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic.
Pavard aliisaidia timu yake ya Taifa France kushinda ubingwa wa kombe la Dunia 2018 na pia alishinda goli bora la michuano hiyo