Tottenham kuhamia uwanja wao mpya
Klabu ya Tottenham Hotspur hatimaye wanajiandaa kuhamia katika uwanja wao mpya na klabu hiyo wanataraji kutoa tangazo hilo katika saa 24 zijazo.
Timu hiyo ipo katika ukaguzi wa mwisho wa uwanja huo huku wakisubiri vyeti vya usalama.
Mechi ya kwanza katika uwanja huo mpya inatarajiwa kuwa mwezi Machi mwaka huu, ambapo Machi 2 Spurs watakuwa wapo nyumbani kucheza na Arsenal.
Inaripotiwa kuwa Spurs hawataki mechi hiyo ya Arsenal ndio iwe ya kufungua uwanja wa mpya kwa kuhofia kupoteza mchezo huo, hivyo wanatazamia kusubiri mchezo wao na Crystal Palace Machi 14 ndio uwe wa ufunguzi.
Tottenham wamekuwa wakitumia uwanja wa Wembley kama uwanja wao wa nyumbani tangu msimu uliopita.