MAURIZIO SARRI KASEMA KWA MTAZAMO WAKE ANAONA FABREGAS AONDOKE
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anaamini kuwa maamuzi ya kumuacha kiungo wa kihispaniola Cesc Fabregas aondoke Chelsea anaamini ni sahihi kwa kiungo huyo na yana faida sana kwa mchezaji huyo kwa siku za usoni, hiyo inatokana na utamaduni au falsafa ya Chelsea.
Maurizio Sarri anasema maamuzi ya kwenda Fabregas katika klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa yana faida zaidi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kwani Chelsea huwa hawampi mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja mchezaji aliyefika umri wa miaka 30 na kuendelea, kwakuwa Monaco wamempa ofa ya mkataba wa miaka miwili ni salama kwake zaidi kwa Fabregas.
“Kwa maoni yangu Fabregas anatakiwa kuondoka Chelsea, unajua kabisa hali, unajua kabisa katika hii klabu kuna sheria kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 30 hawezi kupewa mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja, amepata ofa ya mkataba wa miaka miwili sitaki mchezaji muhimu kama Fabregas awe hana furaha” alisema Maurizio Sarri
Cesc Fabregas aliyebakiza mkataba wa miezi sita Chelsea, aliutumia mchezo wa Kombe la FA kati ya Chelsea dhidi ya Nottingham Forest uliyomalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao 2-0 kuwaaga mashabiki kwani hiyo ndio ilikuwa game yake ya mwisho.