BARCELONA IMEMUWEKEA NGUMU SUAREZ KWENDA ARSENAL
Klabu ya FC Barcelona haitaki kumuachia mchezaji wao Denis Suarez aihame timu hiyo mwezi huu Januari na kwenda katika klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Uingereza, Arsenal wamedhamiria kuhakikisha wanasajili kiungo katika usajili wa dirisha hili dogo la Januari.
Arsenal wamedhamiria kumleta Emirates Denis Suarez mwenye umri wa miaka 25 na tayari wameongea na wakala wa mchezaji huyo na kumwambia kuwa wamemtengea dau la pauni milioni 20 ili wampate kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya kiungo.
Pamoja na jitihada hizo za Arsenal lakini Barcelona tayari wameshaweka wazi msimamo wao hawataki mchezaji huyo aondoke kwa mujibu wa mtandao wa The Mirror, Arsenal wanataka kufanya usajili wa kiungo kama mbadala wa Aaron Ramsey ambaye anaripotiwa kuwa mbioni kuondoka ila walikuwa wanamtazamia kumsajili Ever Banega wa Sevilla akiwa na miaka 30 ila wanaamini Suarez ndio chaguo sahihi zaidi kulingana na umri wake.