Nyoni awapa pigo Simba
Imeripotiwa kuwa kocha wa Simba SC Patrick Aussems amethibitisha kuwa beki Erasto Nyoni hatacheza mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya SJ Saoura ya Algeria jumamosi hii Januari 12 kufuatia kuumia goti lake jana kwenye mechi ya Mapinduzi Cup dhidi ya KMKM visiwani Zanzibar.
Simba SC itaivaa timu hiyo anayoichezea mshambuliaji wa Tanzania Thomas Ulimwengu siku ya jumamosi uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wao wa kwanza katika kundi D.
Kumkosa Nyoni ni pigo kwa kocha huyo kutokana na uwezo na mchango wake katika kikosi cha Simba.