Simba SC kuleta kikosi B Mapinduzi
Baada ya timu ya Simba kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2019 kwa ,kuifunga KMKM katika uwanja Amaan Visiwani Unguja, timu hiyo sasa inasubiri kujua itacheza na nani nusu fainali.
Mwalimu wa Simba SC Patrick Aussems tayari ameoneshwa kusikitishwa kwa kuumia kwa mchezaji wake tegemeo katika kikosi Erasto Nyoni na amethibitisha kuwa sasa wataileta timu yao ya vijana imalize mashindano na wao kwenda kucheza mchezo wa klabu Bingwa Afrika.
“Sijali kuhusu matokeo ninachohofia majeruhi ya Erasto Nyoni ,kuhusu matokeo sijali kwa sababu ninaamini tulikuwa tumeutawala mchezo kwa asilimia kubwa, nimeridhishwa na kiwango lakini nimewaomba wakilete kikosi cha Simba B kumalizia mashindano na niliwaambia kabla ya mchezo kuwa hii ilikuwa zawadi kwao” alisema Patrick Aussem
Simba sasa imelazimika kutangaza mapema kuondoka na kureja Dar es salaam kwa ajili ya kuipeleka timu kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa makundi wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Js Saouro ya Algeria utakaopigwa Jumamosi hii Januari 12 uwanja wa Taifa.