Yahaya Zayd atimkia Misri
Mshambuliaji wa Azam FC Yahaya Zayd amepiga hatua nyingine katika maisha yake ya soka baada ya kuripotiwa kuwa amesafiri usiku wa jana kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Misri kusaini mkataba wa kucheza soka la kulipwa.
Inaripotiwa kuwa Yahaya Zayd anaenda kujiunga na timu ya Ismaily ambayo pia inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi itakayoanza Januari 12, Yahaya Zayd anaenda kusaini mkataba wa miaka mitatu na sio kufanya majaribio.
Hivyo mambo yakienda kama yalivyopangwa mshambuliaji atapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19, Ismaily imepangwa Kundi C na timu za CS Costantine ya Algeria, Club Afracain ya Tunisia na TP Mazembe ya Congo.