Rooney akamatwa tena kwa ulevi
Nahodha wa zamani wa Man United na timu ya Taifa ya England Wayne Rooney alikatamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Dulles jimbo la Virginia nchini Marekani baada ya kukutwa amekunywa dawa za usingizi pamoja na pombe ambapo ilimpelekea kuchanganyikiwa.
Mchezaji huyo alikunywa dawa hizo na pombe wakati akiwa safarini kutoka Saudi Arabia Disemba 16 mwaka jana na hivyo kupelekea kuonekana kuchanganyikiwa alipotua uwanja wa ndege.
.
“ Wayne Rooney alikunywa dawa za usingizi alizoagizwa kuzinywa (na daktari) akachanganya na pombe na hivyo kusababisha kuchanganyikiwa alipowasili uwanja wa ndege “ alisema msemaji wa mchezaji huyo.
Baada ya kukamatwa na polisi Rooney alitozwa dola 25 ( Tsh 50,000) na kuachiwa huru. Januari 4 alitozwa dola 91 ( Tsh 200,000) ambayo ni gharama ya kesi yake.
Rooney ambaye anacheza katika klabu ya DC United ya Marekani, Septemba 2017 alifungiwa kuendesha gari kwa muda wa miaka miwili baada ya kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa huko nchini England.