HII NDIO TIMU INAYOTAKA KUMPA KAZI MOURINHO
Ni siku 18 zimepita toka uongozi wa timu ya Manchester United watangaze kusitisha mkataba wa kazi wa kocha Jose Mourinho kuifundisha timu hiyo na kumtangaza Ole Gunnar kama ndio kocha wao mpya wa muda, leo zimeripotiwa taarifa kuwa Jose Mourinho anajiandaa kupata dili jipya la kufundisha soka.
Imeripotiwa kuwa kocha huyo raia wa Ureno Jose Mourinho, anahitajika na klabu ya Benfica ya nchini kwao Ureno na kutaka kumpa ajira, hivyo kuna uwezekano kabla ya mwezi mmoja kuisha Jose Mourinho kama watafikia makubaliano atapata kazi Benfica.
Kama tetesi hizo zilizotolewa na mtandao wa express.co.uk zitatimia basi Jose Mourinho atakuwa anarudi kuwa kocha wa Benfica kwa mara ya pili, baada ya mwaka 2000 kuwa kocha msaidizi kwa muda mfupi na kumrithi Jupp Heynckes lakini Mourinho hakudumu katika nafasi hiyo alijihudhuru na kuishukuru timu hiyo kwa kumpa nafasi ya kuanza kazi ya ukocha katika maisha yake.
Hata hivyo tukukumbushe tu baada ya Manchester United kutangaza kumfuta kazi Jose Mourinho Desemba 18 2018, walimlipa kocha huyo pauni milioni 22.5 kama fidia ya kuvunja mkataba na mreno huyo, Mourinho akiwa na Manchester United alikuwa analipwa pauni 346,000 kwa wiki.