DIEGO MARADONA KUFANYIWA UPASUAJI
Kocha wa timu ya Dorados ya nchini Mexico na gwiji wa soka wa Argentina Diego Maradona mwenye umri wa miaka 58 kwa sasa inaripotiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufanyiwa upasuaji kufuatia kuugua na kupelekwa hospitali.
Uchunguzi uliofanywa na madaktari unaeleza kuwa gwiji huyo wa soka amegunduliwa kuvuja damu ndani ya tumbo lake hivyo ili kuokoa maisha na kumpatia matibabu ya uhakika atatakiwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo lake.
Watoto wake Gianina, Jana na Diego Junior walikuwa hospitali wakifuatilia hali ya baba yao, Maradona alitangazwa kuwa kocha wa timu ya Dorados mwezi Septemba mwaka 2018, timu hiyo inashiriki Ligi daraja la pili.
Pamoja na kuwa timu anayoifundisha Maradona ilipoteza mchezo wa play off dhidi ya Athletico San Luis mwezi uliopita na kuzima ndoto za timu hiyo kupanda Ligi Kuu, wakala wake Matias Morla alieleza kuwa kocha huyo ataendelea kuifundisha Dorados kwa msimu mwingine tena.