WAKALA WA MCHEZAJI WA THOMAS ULIMWENGU KAMUANDIKIA UJUMBE CHAMA KABLA YA TIMU ZAO KUKUTANA JANUARY 12 2018.
Januari 12, 2019 baada ya miaka 15 wekundu wa Msimbazi Simba SC watapata fursa nyingine ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya JS Saouro katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu kwa timu zote kwa Simba SC na Js Saouro inayochezewa na mtanzania Thomas Ulimwengu, wakala wake ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anakuja Tanzania kuisapoti Js Saouro na kumuomba radhi mchezaji wa Simba Clotus Chama kuwa sasa hivi wapo tofauti.
Wakala huyo wa Ulimwengu anayejulikana kwa jina la Camara Ibrahim ameandika “Natoka Algeria nakuja Tanzania kumsapoti Simba wangu mwenye njaa (akiimaanisha Thomas Ulimwengu) katika mchezo wa Saouro vs Simba SC pole Chama safari hii tupo tofauti” aliandika Camara Ibrahin katika ukurasa wake wa instagram.
Tukukumbushe tu wakala Camara Ibrahimu amekuwa akifanya kazi za uwakala na kumsimamia Ulimwegu katika dili mbalimbali, kwa sasa Camara anakuja na inaweza akaona vipaji vingine na akafanya nao kazi na kuongeza idadi ya watanzania wanaocheza soja nje ya nchi Tanzania.