FA IMEMPA ONYO KOCHA WA MANCHESTER CITY PEP GUARDIOLA
Klabu ya Manchster City kwa sasa imerudi katika furaha ya hali ya juu kufuatia kufufua matumaini ya wao kutetea taji lao Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Liverpool ambao kabla ya mchezo wa jana kukutana dhidi yao Liverpool alikuwa anaongoza kwa tofauti ya alama 7.
Hata hivyo mchezo wa Manchester City dhidi ya Liverpool ulimalizika kwa Manchester City wakiwa kwao Etihad kupata ushindi wa mabao 2-1 na kufanya tofauti ya alama kuwa nne sasa katika msimamo wa Ligi Kuu, Liverpool wakiongoza kwa alama 54 wakifuatiwa na Manchester City wenye alama 50.
Kocha Pep Guardiola katika mchezo huo alifanya tukio ambalo chama cha soka Uingereza FA kimempa onyo kwa kitendo chake cha kuonesha kukasirika na kurusha scarf uwanjani kufuatia muamuzi wa game hiyo kukataa kuipa faulo Manchester ambapo Guardiola alienda kuwaka kwa fourth official Martin Atknson.
