JURGEN KAKASIRIKA VINCENT KOMPANY KUTOONESHWA KADI NYEKUNDU
Baada ya majogoo wa Jijili Liverpool kukumbana na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Etihad, kocha wa klabu hiyo amebadilika na kuwa mbogo kutokana na kushangazwa na nahodha wa Manchester City Vincent Kompany kubaki uwanjani.
Mabao ya Sergio Aguero na Leroy Sane dakika ya 40 na 72 ndio yameifufulia Manchester City matumaini ya kuwania taji hilo, bado la Firmino la dakika ya 64 halikuweza kuisaidia Liverpool kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza.
“Nampenda sana Vincent lakini inakuwaje duniani ile sio kadi nyekundu? Kama watamgonga gonga MO atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima, haikuwa rahisi kwa refa kuona nilichokuwa nakiona” Jurgen Klopp akizungumzia rafu aliyofanyiwa Mohamed Salah na Vincent Kompany kuwa alitakiwa kuoneshwa kadi nyekundu

Liverpool baada ya kufungwa sasa wameweza kuifufua Man City kurudi katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu kwa kuwa sasa wapo tofauti ya alama nne tu huku wote wakiwa wamecheza game 21, Man City akiwa na alama 50 wakati Liverpool wakiwa na alama 50, hivyo wanaweza kuwachanganya zaidi Liverpool wakaingia mkenge wa kupoteza game kadhaa.