MAURIZIO SARRI KATOA KAULI TATA USAJILI WA PULISIC CHELSEA
Kocha mkuu wa timu ya Chelsea Maurizio Sarri amenukuliwa na moja kati ya vyombo vya habari kuhusiana na usajili wa kiungo mpya wa timu hiyo Pulisic mwenye umri wa miaka 20 kusajiliwa kutoka Borussia Dortmund kwa dau la uhamisho wa pauni milioni 58.
Maurizo Sarri ametoa kauli inayoeleza kuwa alikuwa hafahamu chochote kuhusu uhamisho wa Pulisic kutua Chelsea kwa sababu yeye hausiki na masuala ya kufanya usajili wa wachezaji ila anachoweza kusema ni kuwa bodi ya wakurugenzi inajuwa mapendekezo yake katika suala la usajili.
“Sijui chochote mimi sio kiongozi wa masoko au dili la Pulisic hivyo ni vigumu kwangu kuzungumza kuhusiana na hilo, Bodi inajua mapendekezo yangu ila nafikiri tunahitaji kitu cha tofauti kwa ajili ya wasifu huo” alisema Maurizio Sarri

Klabu ya Chelsea jana ilitangaza kuwa imefikia makubaliano ya kumsajili kinda wa USA Pulisic mwenye umri wa miaka 20 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani ila ataendelea kucheza kwa mkopo Dortmund hadi mwisho wa msimu, Pulisic ameichezea michezo 115 Dortmund na kuifungia mabao 15 wakati timu ya taifa ya USA akicheza michezo 20 na kupachika mabao 9.