KOCHA WA MANCHESTER UNITED BADO ANAMUHITAJI SANCHEZ
Kocha wa kipindi cha mpito wa Manchester United Ole Gunnar Solksjaer anaonekana kuendelea kuotesha mizizi ya uhusiano wake kati yake na wachezaji wa timu hiyo, Ole Gunnar Solksjaer inaonekana ameamua kweli kuwashawishi mabosi wa Manchester United wampe kazi ya kudumu.
Baada ya mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez kukutana na wakati mgumu wakati wa utawala wa Jose Mourinho hivyo kocha Ole Gunnar Solksjaer ametoa kauli ambayo inafaida kwa Sanchez lakini inatajwa kuwa inaimarisha uhusiano kati yake na wachezaji.
Ole Gunnar Solksjaer ambaye anapambania kuhakikisha Manchester United inamaliza TOP 4 kama alivyoagizwa na mabosi zake, ameeleza kuwa mabadiliko aliyoyafanya katika kikosi cha Manchester United yatakuwa na faida kwa Alex Sanchez ambaye kwa wiki zilizopita chini ya Jose Mourinho alikuwa na wakati mgumu.
Kabla ya kuondoka kwa Jose Mourinho kulikuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka mwisho wa msimu kutokana na kuwa na mahusiano mabaya na kocha Jose Mourinho, Sanchez amecheza michezo 30 na Manchester United na kufunga mabao manne pekee toka alivyojiunga na timu hiyo Januari 2018 ila kocha Ole Gunnar Solksjaer anasema mchezaji huyo ni muhimu na mabadiko katika kikosi chake yatakuwa na faida kwa nyota huyo.