Oliech atua Gor Mahia
Nahodha wa za zamani wa timu ya taifa ya Kenya Dennis Oliech amejiunga na miamba wa ligi hiyo, Gor Mahia kwa kandarasi ya miaka miwili.
Oliech ambaye mwisho alicheza soka mwaka wa 2015 katika milki ya kiarabu amesaini mkataba ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi katika ligi ya Kenya. Mshahara wake wa mwezi mmoja utakuwa shilingi za Kenya laki tatu na hamsini ( Tsh Milioni 7.8 ).
Atapata shilingi milioni tatu kama ada ya usajili.
.
“Mshambulizi Dennis Oliech amejiunga na kilabu chetu kwa misimu miwili,” ilitangaza Gor Mahia katika taarifa fupi.
Oliech alianzia kandanda yake katika timu ya Mathare United mwaka wa 2003. Baada ya kung’aa alielekea kilabu ya Al Arabi ya Qatar na vilabu vya Nantes, AJ Auxerre na Ajaccio nchini ufaransa.. Alirejea uarabuni mwaka wa 2015 na kujiunga na Dubai CSC lakini aliondoka Dubai miezi michache baadaye.
Katika timu ya taifa, Oliech aliiongoza Kenya kufuzu kwenye Kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2004. Alistaafu kutoka timu ya taifa mwaka wa 2015