Martial ajiondoa katika mitandao ya kijamii
Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Anthony Martial ghafla ameamua kujiondoa katika mitandao ya kijamii pasipo kutajwa kwa sababu zozote za yeye kufikia maamuzi hayo.
Mfaransa huyo ambaye amekuwa na miongoni mwa wachezaji wanaoisaidia timu kwa kuifungia mabao 9 msimu huu, amefuta kurasa zake za mitandao ya kijamii za twitter na instagram, kwa wale ambao walikuwa wamemfuata katika mitandao ya kijamii instagram walikuwa wanakutana na ujumbe unaosema “this page isn’t available “
Wakati waliokuwa wanamfuatilia twitter walikuwa wanakutana na ujumbe “user not found????” utamaduni wa Martial unazua utata, aligonga vichwa vya habari mwezi Mei 2018 alipoamua kufuta picha zake nyingi instagram, hivyo mashabiki wakaanza kuhisi kuwa nyota wao huyo yuko mbioni kuondoka Manchester United.