AMRI SAID KAHAMIA UPANDE WA PILI, MWAKA MPYAA
Aliyekuwa kocha wa timu ya Mbao FC Amri Said ameonesha kuamua kuanza mwaka mpya na mambo mapya baada ya kuamua kusaini na timu mpya hiyo ikiwa ni wiki chache zimepita toka atangaze kuachana na Mbao FC kwa kile kinachoitwa majungu.
Amri Said jana amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ya kukinoa kikosi cha Biashara United ya Musoma ambayo ni majirani na timu ya Mbao FC ambayo inatokea jiji la Mwanza.
Kocha Amri Said anaingia katika timu ya Biashara United ikiwa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu 2018/19, Amri Said akiwa ana jukumu la kupambania timu hiyo isishuke daraja kutokana na kusuasua.
Tukukumbushe tu Amri Said licha ya kuisaidia Mbao ikiwa nafasi za Juu katika Ligi Kuu, aliondoka kutoka na uongozi wa timu hiyo kumleta Kocha Ally Bushiri katika timu hiyo kama msaidizi wake lakini kielemu ya ukocha wote wakiwa daraja B, pendekezo la Amri Said lilikuwa ni kuletewa kocha mwenye daraja A ili awe msaidizi au apewe kocha mweny daraja C awe msaidizi wake.