KMC, MTIBWA NA SINGIDA ZILIPIGWA CHINI KOMBE LA MAPINDUZI 2019
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya Kombe la Mapindizi Hamis Said amezungumzia uamuzi wao wa mwaka huu wa kuchezesha timu 9 katika michuano hiyo na Tanzania bara kuzichukua timu tatu.
Hamis Said ameeleza kwa mwaka 2019 michuano hiyo imekumbwa na changamoto kubwa kwa vilabu vya kigeni kukubali mualiko lakini wamenyimwa ruhusa na mashirikisho ya mpira wa miguu ya nchini kwao, kamati ya Mapinduzi ililenga kuialika URA ya Uganda ambayo ilinyimwa ruhusa na Bandari ya Kenya pia.
.
Kwa upande wa Tanzania bara wamezialika timu tatu kutokana na uhaba wa viwanja na muda hivyo pamoja na timu za Singida United, Mtibwa Sugar na KMC ziliomba nafasi hiyo lakini walishindwa kuzipa nafasi hiyo kutokana na muda kuwa mchache wa mashindano.