MWINYI ZAHERA ATOA SIRI ZA MAKAMBO KUFUNGA MABAO TPL
Jina la Mkongomani anayekipiga katika timu ya Dar es Salaam Young Africans Herietier Makambo limekuwa gumzo kila kona kutokana na mchezaji huyo kuwa mahiri uwanjani katika suala zima la kupasia nyavu hususani anapokuwa ameingia eneo la hatari anakuwa makini zaidi.
Makambo ambaye ni raia wa Congo ni moja katia ya wachezaji wa Yanga wanaounda safu ya ushambuliaji ya kikosi hiko na amekuwa msaada mkubwa katika kufunga mabao, hadi sasa Makambo ameifungia Yanga jumla ya mabao 11 katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye nae ni raia wa Congo na Ufaransa ameeleza siri ya Makambo kuwa mahiri katika kufumania nyavu zaidi uwanjani.
“Makambo anapenda ugali sana ndio chakula anapenda na mimi namwambia kama unakula ugali hakuna shida mimi naomba uwanjani uwe hivi, mimi namjua Makambo toka tupo Congo anacheza Lupopo anafunga hat-trick TP Mazembe sasa atakuja kushindwa kufunga magoli hapa” alisema MwinyI Zahera katika mahojiano maalum na Azam TV
Yanga sasa bado ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa sasa msimu wa 2018/2019 wakiwa na jumla ya alama 50 walizokuwa wamevuna katika michezo 18 ya Ligi Kuu,, wanaowafutia ni Azam FC wakiwa na jumla ya alama 40 walizovuna katika michezo 17 na Simba nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 33 na viporo vine.