Mkenya Nam ajiunga na Vipers
Mabingwa wa Uganda Vipers wamemteua Mkenya Michael Nam Ouma kama kocha mshikilizi baada ya Javier Espinoza kupigwa kalamu.
Espinoza alifutwa kazi siku ya jumamosi na sasa Nam ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka kumi na saba ataiongoza timu hiyo kwa muda.
“Kocha wetu mpya ni Mkenya Michael Ouma ambaye ndio kocha mkuu. Atasaidiwa na Moses Oloya ambaye ni kocha wa walinda lango. Edward Ssali atakuwa mkuu wa mazoezi naye Ram Nyakana ataongoza kitengo cha nguvu na uvumilivu,” Vipers ilitangaza.
Nam ambaye ashawai ifunza timu za Posta Rangers, FC Talanta, Karuturi Sports na Agro Chemicals ana leseni ya CAF A.
Anakuwa kocha wa kwanza mwenye asili ya Kenya kwa miaka ya karibuni kuteuliwa kama kocha mkuu nchini Uganda.
Kwenye kilabu ya Vipers, atajiunga na Mshambulizi wa Kenya Noah Wafula ambaye anaichezea Vipers.