N’golo Kante apeleka Pointi 3 kwa Sarri
Goli la N’golo Kante katika dakika ya 51 dhidi ya Crystal Palace leo limeipa pointi tatu Chelsea, wakiibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo huo waliocheza katika uwanja wa ugenini.
Ushindi huo unawafanya Chelsea kufikisha pointi 43 na kumaliza mwaka 2018 wakiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England.
Kikosi hicho cha Muitalia Maurizo Sarri kitashuka dimbani tena Januari 2 ambapo watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuwakaribisha Southampton.