KOCHA WA SIMBA KAWATOA HOFU MASHABIKI BAADA YA MAKUNDI KUPANGWA YA KLABU BINGWA
Droo ya Makundi ya michuano ya klabu Bingwa
Afrika ilichezeshwa Ijumaa ya Desemba 28 2018 na
makundi manne kujulikana, droo hiyo ilichezeshwa
nchini Misri Cairo ambako ndio makao makuu ya
shirikisho la mpira wa miguu Afrika yalipo Tanzania
ikiwakilishwa na timu moja ya Simba SC.
Baada ya droo kuchezeshwa mbele ya viongozi
mbalimbali wa vilabu shiriki ikiwemo wa CAF, Simba
yenyewe iliwakilishwa na Salim Abdallah ‘Try Again’
katika upangaji wa makundi hayo na kujikuta
wameangukia Kundi D lenye timu za Al Ahly ya Misri,
AS Vita Club ya Congo na JS Saoura ya Algeria.
Kila mtu amekuwa na mtazamo wake kuhusiana na
Kundi walilopangwa Simba kuwa jepesi na wengine
wanasema gumu kutokana na kupangwa na vigogo
wa soka wa Misri Al Ahly ambao wamekuwa
wakisumbua sana soka la Afrika, kocha wa Simba
Patrick Aussems amekuwa na mawazo tofauti na
kuandika kuwa kwa mtazamo wake yeye kila timu ina
nafasi Kundi hilo wala sio gumu.
“Ili Kundi lipo wazi sana kwa timu zote na kiukweli
tuna nafasi ya wazi ya kuingia hatua ya robo fainali
wacha tushikamane” maneni ya Patrick Aussems
kupitia ukurasa wake wa Twitter.
