CHELSEA IMEMRUDISHA JOE COLE BAADA YA MIAKA NANE
Baada ya kucheza ndani ya Chelsea kwa misimu saba
Joe Cole ameamua kurudi tena Chelsea kwa namna
nyingi, Joe Cole anarudi Chelsea sio kama mchezaji
tena kama ilivyokuwa awali lakini anarejea katika
klabu hiyo kama kocha wa Academy ya Cheslea.
Joe Cole ambaye ametangazwa na Chelsea leo kurudi
kama kocha wa academy alikuwa akiichezea Chelsea
kuanzia mwaka 2003 alipojiunga na timu hiyo
akitokea West Ham United hadi mwaka 2010
alipoamua kuondoka na kwenda kujiunga na timu ya
Liverpool.
Cole akiwa na Chelsea alifanikiwa kupata mafanikio
mbalimbali na amefanya mengi katika soka hadi pale
mwaka 2018 alipoamua rasmi kustaafu kucheza soka
la ushindani 2018 akiwa na umri wa miaka 37, Cole
timu yake ya mwisho kucheza kabla ya kustaafu
ilikuwa ni Tampa Bay Rowdies ya Marekani kabla ya
hapo Cole amewahi kucheza katika vilabu vya Lille ya
nchini Ufaransa, Aston Villa ya nchini Uingereza na
Coventry City ya nchini kwao Uingereza pia.