SERIE A WAMEIADHIBU INTER MILAN KISA KOULIBALY
Siku ya kusherekea kufungua zawadi (Boxing Day) Ligi Kuu ya nchini Italia iliendelea kama kawaida kwa michezo mbalimbali kuchezwa nchini Italia lakini kubwa ni matukio yaliojitokeza katika mchezo wa Napoli dhidi ya Inter Milan uliyochezwa katika uwanja wa Sansiro.
Mchezo huo uliomalizika kwa Napoli kupoteza kwa bao 1-0, kulitokea kitendo cha ubaguzi wa rangi kwa mlinzi wa kati wa Napoli raia wa Senegal, Kalidou Koulibaly, kitendo ambacho kiliufanya mchezo huo kuwa gumzo mtandaoni.

Serie A leo wamewafungia michezo miwili ya Ligi Kuu Italia timu ya Inter Milan kucheza michezo yake miwili mfululizo ya nyumbani pasipo uwepo wa mashabiki uwanjani ambao ndio baadhi yao walionesha kitendo cha ubaguzi uwanjani, hata hivyo Inter Milan wanapanga kujiandaa kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Wachezaji mbalimbali kama Mohamed Salah na Sadio Mane wa Liverpool, Mario Balotelli wa Nice na Cristiano Ronaldo wameoneshwa kuguswa na kukemea kitendo alichofanyia Koulibaly kuwa sicho cha kiuanamichezo.