MESSI AMETAJA SWALI ANALOULIZWA NA MWANAE IKITOKEA HAWAJASHINDA GAME
Nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi ameamua kuweka wazi changamoto anazikutana nazo kutoka kwa mtoto wake kwanza wa kiume Thiago Messi, nyota huyo wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina ameweka wazi maswali ambayo amekuwa akiulizwa na mwanae kuhusu soka.
Messi ana watoto watatu ila mara nyingi amekuwa na utamaduni wa kupenda kutembea na mwanae mkubwa zaidi Thiago na kwenda nae sehemu mbalimbali kama uwanjani kuagalia mechi lakini mwanae amekuwa na utamaduni wa kumuhoji baba yake na kutama aelezewe kwa nini timu yao (Barcelona) imefungwa siku hiyo.
“Thiago Messi amekuwa na utaratibu wa kunilazimisha nimuelezee mawazo yangu kuhusiana na kilichotokea uwanjani hususani kwa nini hatujashinda katika mchezo huo” alisema Lionel Messi kuhusiana na maswali ya mwanae Thiago wakiwa nyumbani baada ya kuwa Barcelona haijapata matokeo mazuri au imefungwa.
Tukukumbushe Lionel Messi mwenye umri wa miaka 31 amebahati kupata watoto wa tatu wa kiume Thiago, Ciro na Mateo kutoka kwa mkewe Antonella lakini mwanae Thiago wa kwanza mwenye umri wa miaka 6 amekuwa akiongozana nae sehemu mbalimbali.