Pogba anategemea zawadi ya mtoto kutoka kwa mpenzi wake
Mpenzi wa Paul Pogba mwanadada Maria Salaues alikuwa ni miongoni mwa washangiliaji 75,000 ambao walikuwa katika uwanja wa Old Trafford jana Disemba 26 kushuhudia mechi kati ya Man United na Huddersfield.
Wakati mwanadada huyo,23, akiingia uwanjani, alionesha tumbo lake la ujauzito na kuonesha kuwa sasa mambo kwa Paul Pogba ni mazuri ndani na nje ya uwanja.
Pengine uwepo wake uwanjani uliongeza hamasa kwa mpenzi wake dimbani ambaye alifunga goli mbili katika ushindi wao wa 3-1, ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa kocha mpya wa United Ole Gunnae Solskjaer.
Katika mechi mbili zilizopita Paul Pogba ambaye alikuwa na ugomvi na kocha aliyepita Jose Mourinho , amefunga goli mbili na kutoa pasi za mabao mbili.