Ratiba ya Mapinduzi Cup 2019 yatoka, Simba na Yanga ndani
Michuano ya mapinduzi Cup itaanza kutimua vumbi Januari Mosi mpaka Januari 13, 2019 visiwani Zanzibar, ambapo ratiba yake ikiwa tayari imetolewa na vigogo wa soka nchini Simba na Yanga zikiwa katika makundi mawili tofauti .
Katika michuano hiyo ambayo huchezwa mwezi Januari kila mwaka, Kundi A lina timu za Chipukizi, Mandege, KMKM, na Simba, wakati kundi B limesheheni timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.
Kamati ya michuano hiyo imetangaza kuongeza zawadi za washindi, ambapo sasa mshindi wa kwanza atakuwa akipata shilingi milioni 15 za Tanzania badala ya milioni 10, na mshindi wa pili ambaye alikuwa anapata milioni 5, sasa atapata milioni 10.
Kwa mujibu wa kanuni za michuano, endapo Azam fc watachukua kombe hili msimu huu, wataondoka nalo moja kwa moja kwani watakuwa wamechukua mara 3 mfululizo.