HAJI MANARA KAWAPA ONYO WACHEZAJI WA SIMBA SC
Siku moja baada ya klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kufanikiwa kuvunja rekodi yao ya kutolewa na klabu ya Nkana FC katika michuano ya CAF kwa kuwafunga 3-1 na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2018/2019, msemaji wao Haji Manara kafunguka.
Haji Manara kupitia mahojiano maalum na Azam TV amefunguka na kueleza kuwa wachezaji wao hawatakiwi kujisahau baada ya ushindi huo, kwa sasa wanatakiwa mchezo ujao wa Kombe la Azam Sports Federation dhidi ya timu ya Mashujaa ya Kigoma kwani sio wakuwachukulia poa.
“Timu kubwa inapaswa kuonesha ukubwa wake kila mechi kama jana tumeweza kuwafunga timu ya Nkana Red Devils timu kubwa kabisa ya Zambia goli 3-1, tusije kudharau mtu yoyote anayekuja, kwa wachezaji wanalijua hilo na sisi tunalijua hilo kwamba lazima tuwachukulie mashujaa kama mkubwa mwenzetu tukiwachukulia tunacheza na timu dhaifu yatatukuta yale ya Green Warriors”alisema Haji Manara
Simba SC wakati ikisubiri kupangwa kwa makundi ya kombe la Klabu Bingwa Afrika siku ya Desemba 28 na kufahamu imepangwa na timu gani kati ya 16 zilizoingia hatua hiyo, sasa wana kazi ya kucheza mchezo wa Kombe la ASFC dhidi ya Mashujaa tarehe 26 na msemaji wao amewasihi kuwa makini yasije yakawakuta ya mwaka jana walivyotolewa na Green Warriors kwa penati.