PIGO ARSENAL ITAMKOSA MKHITARYAN KWA WIKI SITA
Mtandao mahiri wa habari za michezo nchini Uingereza wa dailymail umeripoti taarifa za kushitusha kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal kufuatia pigo walilolipata kutoka kwa kiungo wao Henrikh Mkhitaryan kuumia na kudaiwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda kidogo.
Henrikh Mkhitaryan anaripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki zisizopungua sita kufuatia jeraha la kuumia mguu alilolipata wakati wa mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Tottenham uliomalizika kwa Arsenal kupoteza, Mkhitaryan alicheza kwa dakika 45 za kwanza na kutolewa nje ya uwanja kabla ya kuukosa mchezo wa Ligi Kuu wa ushindi kwa Arsenal dhidi ya Burnley.
Arsenal wamezithibitisha taarifa hizo kupitia tovuti yao na kueleza kuwa kiungo wao raia wa Armenia mwenye umri wa miaka 29 hatakosekana uwanjani kwa wiki kadhaa, Mkhitaryan atakuwa kamili kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kabla ya kuanza kucheza mechi baada ya wiki sita.