HASSAN KESSY KAWAPA USHAURI WA SIMBA BAADA YA KUITOA TIMU YAKE
Timu ya Nkana Red Devils ikiwa kwenye ardhi ya Tanzania siku ya Jumapili ya Desemba 23 imeondolewa rasmi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu wa 2018/2019 dhidi ya wenyeji wao Simba SC, Nkana wameondolewa baada ya Simba SC kupindua matokeo ya mchezo licha ya awali Nkana kutangulia.
Mbao 3-1 ya Simba yaliofungwa na Jonas Mkude, Meddie Kagere na Clotous Chama yameiondoa Nkana licha ya kupata bao la mapema kabisa dakika ya 1y kupitia kwa Bwalya, mchezo ulikuwa na presha kwa Simba baada ya kuingia uwanjani wakijua kuwa wapo nyuma kwa bao 2-1 kutokana na nchezo wa kwanza Zambia walikubali kupoteza.
Kama ufahamu Nkana walikuwa na mchezaji mmoja mtanzania Hassan Kessy ambaye amewahi kuichezea Simba, hivyo baada ya mchezo na timu yake kuiaga michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2018/2019 alihojiwa na Azam TV na kusema kuwa Simba wamerekebisha makosa yao na kupata matokeo lakini wanachoka sana hivyo wanapaswa wajiandae zaidi huko waendako.
“Hakuna kilichochangia sisi kupoteza mchezo wenyewe tu tumetengeza nafasi nyingi na tumeshindwa kuzitumia, hakuna cha tofauti walichokionesha sema wametumia nafasi nyingi walizozipata na kupata matokeo, napenda kuwashauri Simba wajipange vizuri ili wanapoenda katika mashindano wafanye vizuri lakini Simba wanakata sana upepo yaani wanachoka sasa hawako vizuri zaidi wajiandae wanakokwenda” aliseama Hassan Kessy