SAMATTA KIUKWELI HASHIKIKI KWA SASA
Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji bado inaendelea na Desemba 23 vinara wa Ligi hiyo KRC Genk walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa 20 wa Ligi Kuu Ubegji na wenyeji wao KAS Eupen wanaoshika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Ku nchini Ubelgji maarufu kama Jupiter Pro League wakiwa na alama 22.
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kinara wa magoli wa Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji Mbwana Samatta alikuwa sehemu ya kikosi cha timu yake ya KRC Genk kilicheza mchezo huo katika uwanja wa ugenini.
Samatta ambaye ana siku tatu toka asaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia KRC Genk ya nchini Ubelgji kwa miaka miwili zaidi, ndio alikuwa mkuki wa sumu kwa KAS Eupen, kwani ndio mchezaji pekee aliyefunga magoli ya ushindi ya Genk dakika ya 13 na 20 katika ushindi wa mabao 2-0 na kuifanya KRC Genk kuendelea kuongoza Ligi wakiwa na alama 45 wakifuatiwa ba Club Brugge wenye alama 38.
Mabao hayo ni kama zaidi ya Birthday kwake kwani amefunga siku ya Desemba 23 ikiwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzalia na ndio siku waliyocheza mchezo huo, mabao hayo yanamfanya Samatta kuendelea kuongoza katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya ufungaji bora Ligi Kuu Ubelgiji kwa kufikisha jumla ya mabao 14, akiwa mbele kwa mabao matatu zaidi dhidi ya Ivan Santini na Landry Dimata wote wakicheza Anderletch wakiwa na mabao 11 kila mmoja wao.