Simba yatinga makundi klabu bingwa Afrika
Klabu ya Simba imefanikiwa kuwatoa Nkana FC na kujiandikishia tiketi ya kucheza makundi klabu bingwa Afrika baada ya kuifunga kwa goli 3 – 1.
Nkana FC ndio walikuwa wa kwanza kujiandikishia goli lake la kwanza kupitia mchezaji wake machachari Bwalya 17′, Jonas Gerrad Mkude alirejesha matumaini ya wanamsimbazi kwa shuti la mbali ambalo lilikwenda golini na kumshinda mlinda mlango wa Nkana FC 29′, 45′ + 1′ kuelekea kipindi cha mapumziko Meddie Kagere aliwahakikishia wanaSimba kuwa siku ya leo ilikuwa Kufa na kupona kweli kwa kuweka goli zuri la kichwa. Kipindi cha pili kikikaribia kumalizika Mwamba wa Lusaka Chama akaiandikia Simba tiketi ya kuketi kwenye makundi klabu bingwa Afrika 89′
Tukukumbushe tu mchezo wa kwanza kati ya Nkana dhidi ya Simba uliochezwa nchini Zambia ulimalizika kwa 2-1 na hivyo matokeo ya leo yamefanya kikosi cha Simba kushinda kwa jumla ya goli 4-3 dhidi ya Nkana