Ole Gunnar Solskjær Kaanza kauli za mbwembwe mapema
Kocha mpya wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjær ameonekana kuwa na wakati mzuri ndani ya klabu ya Manchester United kufuatia ushindi mnono alioupata kama kocha wa Manchester United katika mchezo wake wa kwanza kama kocha wa timu hiyo.
Mtihani wa kwanza wa Ole Gunnar Solskjær kama kocha wa Manchester United ulikuwa dhidi ya Cardiff City ugenini, timu ambayo imewahi kufundishwa na Ole Gunnar Solskjær kama kocha mwaka 2014, Ole Gunnar Solskjær amepata ushindi wa mabao 5-1, mabao hayo yakifungwa na Marcus Rashford dakika ya 3, Ander Herrera dakika ya 29, Anthony Martial dakika ya 41 na Jesse Lingard aliyepasia nyavu mara mbili dakika ya 57 kwa penati na 90.
Cardiff ambao wamevuna bao moja pekee kwa penati dakika ya 38 kupitia kwa Camarasa bado wanaendelea kuwa na hali mbaya kwakuwa na alama 14 na wapo nafasi nne za chini, yaani wanakaribia nafasi za kushuka daraja, Manchester United wao wanabaki nafasi ya 6 licha ya kuongeza alama tatu ila wanakazi ya kuifukuzia Arsenal walipo nafasi ya tano kwa kuwazidi kwa tofauti ya alama 8, Manchester wakiwa na alama 29.
Baada ya mchezo huo kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjær alinukuliwa akitoa kauli ya kujiamini na itafsiriwa na baadhi ya watu kama tambo kejeli baada ya kusema “Mpira ni rahisi sana kama umepata wachezaji wazuri” alisema Ole Gunnar Solskjær