LIVERPOOL WASHINDWE WENYEWE, ROY HUGSON KAMPA ZAWADI YA CHRISTMAS JURGEN KLOPP
Timu ya Crystal Palace leo imefanikiwa kuzima jiji la Manchester baada ya kufanikiwa kuwafunga Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza Manchester City, Crystal Palace wanakuwa gumzo kufuatia kuonekana kufanikiwa kupata matokeo chanya dhidi ya Manchester City ambao wanaonekana ni wagumu kufungwa hususani katika uwanja wao wa Etihad.
Crystal Palace licha ya ugeni na kuwa na idadi ndogo ya mashabiki katika uwanja wa Etihad, wamefanikiwa kutoka na alama tatu kwa kuwafunga Manchester City kwa mabao 3-2, mabao ya Crystal Palace yakiwekwa nyavuni na Schlupp dakika ya 33, Townsend dakika ya 35 na Milivojevic kwa penati dakika ya 55, Man City walipata mabao mawili kupitia kwa Gundogun dakika ya 27 na Kevin De Bruyne dakika ya 85.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Manchester City kufungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu, hivyo matokeo hayo yanamfanya Liverpool wapumue kwa raha kileleni kwa kuwa wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama nne, dhidi ya Manchester City ambao wanabaki na alama zao 44 na Liverpool 48.
Crystal Palace leo ushindi huo umewafanya wapande hadi nafasi ya 14 kwa kufikisha alama 18, wengi wameanza kuleta utani kutokana na ushindi huo kwa Crystal Palace kuwafunga Manchester City nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28, mara ya mwisho Crystal Palace kuifunga Manchester City nyumbani kwake ilikuwa mwaka 1990 ambapo ni msimu ambao Liverpool walikuwa Mabingwa, hivyo ni kama ishara ya Liverpool kutabiriwa Ubingwa mwingine na Crystal Palace.