Mtibwa yatupwa nje kombe la shirikisho Afrika
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika Mtibwa Sugar wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kupoteza michezo yote miwili dhidi ya KCCA ya Uganda.
Mechi ya kwanza ambayo ilipigwa Uganda wiki iliyopita Mtibwa walifungwa kwa goli 3-0 na leo katika mechi ya marudiano iliyopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi timu hiyo kutoka Turiani imeshindwa kufurukuta na kupoteza kwa goli 2-1.
KCCA ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 28 kabla ya Mtibwa Sugar kusawazisha katika dakika ya 51 .
Allan Okello dakika ya 87 wakaandika goli la pili na kujihakikishia ushindi, hivyo kufuzu raundi inayofuata kwa uhakika.