Mh. Joseph Kakunda kuwa mgeni rasmi Simba ikivaana na Nkana FC
Klabu ya Simba imetoa taarifa kwa vyombo vya habari na kuujulisha umma kuhusiana na mgeni rasmi siku ya kesho kuwa anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Joseph Kakunda.
Kikosi cha Simba kesho kitashuka dimbani kupeperusha bendera ya Tanzania dhidi ya Nkana FC inayopeperusha bendera ya Zambia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika
