Chama atimiza ndodo ya shabiki wake
Kiungo aliyejizoelewa umaarufu mkubwa kwenye kikosi cha Simba kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi ya kiungo vyema Clatous Chama ‘Tpipple C’ leo amemkabidhi zawadi ya jezi shabiki wa klabu ya Simba na kwake pia Bw. Raphael Oleshang’ai maarufu kama Mtakatifu Jr baada ya siku kadhaa zilizopita picha yake kusambaa katika mitandao ya kijamii akimuomba Chama ampatie jezi yake.
