ALLAN WANGA ANAINGIA KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI WENYE ELIMU
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Azam FC na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Allan Wanga ameingia katika orodha ya wanasoka wachache dunini wenye elimu ya juu, Wanga anafanikiwa ku-balance yaani kuwa mwanasoka mahiri lakini kuwa na elimu ya juu.
Jana Desemba 21 2019 Allan Wanga ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 33, amefanikiwa kuhitimu chuo Kikuu cha Nairobi stashahada ya rasilimali watu (Diploma of Human Resources) maamuzi ya Wanga yanamuweka pazuri katika kesho yake baada ya maisha ya soka.
Wanga kwa sasa anacheza soka katika timu ya Kakamega Home Boys na amemuoa mwandishi wa NTV ya nchini Kenya Brenda Mulinya Wanga, mshambuliaji huyo aliwahi kusikika kuwa marehem mama yake hakutaka acheze mpira zaidi ya kusoma, Wanga ambaye amewahi kucheza Tusker FC na Azam FC kwa sasa anakuwa katimiza mapendekezo ya mama yake.