JUMA KASEJA KAFICHUA SIRI YA KUJIITA COPER 1 (ONE)
Nahodha wa klabu ya timu ya KMC ya Kinondoni Juma Kaseja ameamua kufunguka kuhusiana nakujipa AKA ambayo imekuwa maarufu lakini wengi wamekuwa hawafahamu hasa mlinda mlango huyo mahiri aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ana maana gani na jina hilo.
Kaseja baada ya mchezo huo wa Kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya timu yake ya KMC dhidi Tanzania Prisons uliyomalizika kwa KMC kutinga hatua inayofuata kwa kuitoa Prisons kwa matuta 4-3, baada ya dakika 0-0 kumalizika ikiwa sare tasa ya 0-0, Kaseja amehusika katika ushindi huo kwa kiasi kikubwa baada ya kudaka penati ya Jeremiah Juma.
“Tunashukuru Mungu kwa kuweza kupata matokeo katika mchezo wa leo na mwalimu alituambia mchezo ni mgumu na ndicho tulichokuja kukutana nacho uwanjani na kwenda katika mikwaju ya penati, Kwa nini Cooper One? Kumekuwa na maneno mengu kuwa Kaseja Kaseja kazeeka Kazeeka kwa hiyo ni meseji tosha kuwa Cooper One haipotei”alisema Juma Kaseja
Tukukumbushe tu Juma Kaseja ni miongoni mwa Kundi la wachezaji wengi waliokuwa zao la shule ya Kijeshi ya Makongo ambayo imekuwa na utamaduni wa kuzalisha wachezaji wa Ligi Kuu kama Jerson Tegete, Amri Kiemba, Henry Joseph na wengine wengi, Kaseja pia amewahi kucheza vilabu vikubwa hapa nchini Vya Simba na Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania kama mlinda mlango namba moja.