KWA MWENDO HUU MANCHESTER CITY WANA KAZI KUISHUA LIVERPOOL
Kuna uwezekano mkubwa sana Liverpool wanafahamu changamoto ya kupata nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza, hiyo inatokana na timu hiyo kuwa na ushindani mkubwa kiasi cha timu ikipoteza mchezo mmoja tu inaweza kuondoka kwenye ramani ya kupoteza nafasi ya kuwania Ubingwa.
Liverpool wanaonekana kulitambua hilo ndio maana usiku wa Desemba 21 2018 ilikuwa inacheza ugenini dhidi ya Wolves mchezo wake wa 18 wa Ligi Kuu lakini haijafanya makosa na kuhakikisha inaondoka na alama zote tatu, Liverpool dhidi ya Wolves wamepata ushindi wa mabao 2-0, mabao yakifungwa na Mohamed Salah dakika ya 18 na beki wao mwenye rekodi zake Van Dijk dakika ya 68.
Ushindi huo umemfanya Van Dijk kugonga vichwa vya habari kutokana na mchezaji huyo kuwa na msimu mzuri zaidi na Liverpool, Van Dijk akicheza mchezo wake wa 32 kama beki wa Liverpool akiwa katika safu ya ulinzi aliruhusu mabao 17 na kucheza mechi 17 bila kuruhusu goli hata moja (Clean sheet). Ushindi huo umedhihirisha kuwa Liverpool wana uhakika wa kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu wakati wa sikukuu ya Christmass kwa ushindi huo kuwafanya wafikishe jumla ya alama 48 katika michezo 18 wakiwazidi Manchester City mchezo mmoja ambao wana alama 44 wakiwa wamecheza michezo 17 hivyo