Leopards wamnyaka Kaheza
Mshambuliaji wa timu ya Simba SC amejiunga na miamba wa Kenya, AFC Leopards kwenye mkopo hadi mwisho wa msimu.
Kaheza ambaye aliingia Simba mwezi Juni hajakuwa akitumika na Mwabingwa hao wa Tanzania na Wameamua kumtuma Kenya kwa mkopo.
Wachezaji wengine wanne pia wameelekea nje kwa MKOPO. Mohamed Rashid ameelekea KMC, Said Nduda amekwenda Ndanda FC na Salum Juma Ishaka ameenda Ashanti FC.
Raia wa Burkina Faso, Zane Coulibaly amejiunga na Simba.
“Tumewapeleka kwa mkopo wachezaji wetu wanne katika klabu kadhaa na wachezaji hao ni Marcel Kaheza – AFC Leopards ya Kenya, Mohammed Rashid – KMC. Said Nduda – Ndanda FC na Salum Juma Ishaka wa under 20 anaekwenda Ashanti FC ya Ilala,”ilisoma taarifa kutoka Simba. .
Pia kama mnavyojua Simba imesajili mchezaji mmoja tu katika dirisha dogo ambae ni Zane ‘CAFU ‘Coulibaly raia wa Burkina Faso toka klabu ya Asec ya Ivory Coast.