Yanga yaendeleza vipigo ligi kuu, yamchapa African Lyon 1-0
Kikosi cha Yanga leo kimefanikiwa kuendeleza uhakika wa kuendelea kukikalia usukani kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuifunga klabu ya African Lyon goli 1-0.
Goli pekee kwenye mchezo wa leo lililoipatia pointi 3 muhimu klabu ya Yanga lilifungwa na Abdallah Shaibu katika dakika ya 64 kipindi cha pili.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru na shabiki mkubwa na aliewahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Muro kupitia ukurasa wake wa Instagram alikipongeza kikosi cha Yanga huku akisisitiza michezo kutumika katika kukuza utalii wa ndani.
Sasa kikosi cha Yanga kinaongoza katika msimamo wa ligi kuu kikiwa na jumla ya alama 47 huku kikiwa kimecheza michezo 17