Vita ya Pogba na Mourinho si ya kitoto
Kwa mujibu wa mtandao wa the sun imeripotiwa kuwa baada ya Jose Mourinho kufukuzwa Man United, kiungo Paul Pogba akiwa mazoezini juzi mazoezini alikuwa akishangilia kwa kupiga kelele huku akisema “ Alifikiri anaweza kunifanya mimi mjinga na kuwabadili mashabiki wawe dhidi yangu . Alicheza na mtu sie “
Inadaiwa kuwa mchezaji pekee ambaye hakushiriki sherehe hizo za kufukuzwa kwa Jose Mourinho ni Romelu Lukaku tu.
Lukaku alisajiliwa na Jose Mourinho mwaka 2017 kwa ada ya pauni milioni 75.
Kwa mujibu wa the sun, mwezi Oktoba mwaka huu katika kikao cha timu, Jose Mourinho alimshauri Paul Pogba anatakiwa ajaribu kuwa kama Frank Lampard.
Badala ya kuchukua ushauri wa Jose, Pogba akiwa na hasira alimuuliza Mourinho kuwa kama Frank Lampard alishawahi kuchukua ubingwa wa kombe la Dunia.