Piers Morgan avalishwa jezi ya Spurs
Mchezaji wa zamani wa Tottenham Peter Crouch na shabiki mkubwa wa Arsenal, mwandishi wa habari Piers Morgan jana wali-bet katika mechi kati ya timu zao.
Walibet kuwa ambaye timu yake itapoteza atavaa jezi ya mpinzani wake wakati wa kuchezesha droo ya nusu fainali ya Carabao Cup.
Katika mchezo huo wa robo fainali uliopigwa Emerates Stadium, Arsenal walichezea kipigo cha goli 2-0 na kutupwa nje ya michuano.
Hivyo Piers Morgan akawa amepoteza bet dhidi ya Crouch na kuvaa jezi ya Spurs wakati droo ya nusu fainali ikifanyika.