Leopards yamtema Odera
Mshambulizi wa timu ya AFC Leopards Ezekiel Odera ameondoka na kujiunga na timu ya KCB kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Hii ni baada ya mshambuliaji huyo mkongwe kuelezwa kuwa haihitajiki kwenye timu ya Leopards kutokana na mazoea yake ya kutohudhuria mazoezi.
Odera akimkasirisha kocha wa Leopards Nikola Kavazovic mwezi Novemba kwa kukosa mazoezi mara kadhaa bila sababu nzuri na hapo ndio kocha huyo alimfukuza mazoezini.
Licha ya kuwa na upungufu kwenye sehemu ya mashambulizi, Ingwe haikuwa na budi kumwachilia Mwana kandanda huyo ambaye amechezea vilabu kadhaa nchini Kenya.
Ashawahi ichezea vilabu vya Gor Mahia, Ushuru, Thika United, Nairobi City Stars na KCB katika hawamu mbili.
Odera ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa Leopards msimu uliopita baada ya kutia kimyani mabao 13.