Simba yakila kiporo chake cha kwanza kwa 2-1
Kikosi cha Simba leo kimeshuka dimbani kucheza mchezo wake wa 13 ikiwa ni jumla ya michezo 3 nyuma ya watani wake wa Jadi Yanga.
Katika mchezo wa leo kikosi cha Simba kimejizolea alama 3 na ushindi wa magoli 2 -1, magoli yaliyofungwa na Adam Salamba 11′ na Said Ndemla 14′ kipindi cha kwanza. Kikosi cha KMC kilipata goli la kufutia machozi katika kipindi cha pili kupitia James Msuva 67′
Kikosi cha Simba sasa kinafikisha jumla ya alama 30 ikishikilia nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Kikosi cha Simba kinatarajia kushuka tena dimbani siku ya Jumapili kuwakabili Nkana FC kutoka Zambia katika michuano ya klabu bingwa Afrika huu ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza klabu ya Simba kupoteza kwa 2-1 nchini Zambia