Solskjær arejea kivingine Old Trafford
Baada ya jana kutangaza kumtimua kocha Jose Mourinho, leo klabu ya Man United wamemtangaza mshambuliaji wao wa zamani Ole Gunnar Solskjær kuwa kocha wao wa muda mpaka mwisho wa msimu huu.
Solskjær ambaye ameichezea Man United kati ya mwaka 1996 na 2007 akifunga goli 126 katika mechi 366, ataungana na Mike Phelan katika kazi hiyo, pamoja na Michael Carrick na Kieran McKenna.
Mechi yake ya kwanza Solskjaer itakuwa ni jumamosi hii dhidi ya Cardiff, timu ambayo aliwahi kuifundisha mwaka 2014 na kushuka nayo daraja kutoka ligi kuu mpaka Championship na baadae kutimuliwa kufuatia kuanza msimu wa Championship vibaya.