Pogba kupigwa faini na Man United
Klabu ya Man United imeripotiwa kuwa inataka kumpiga faini kiungo wao Paul Pogba kufuatia ku-post picha isiyo na heshima kwenye akaunti yake ya instagram muda mchache baada ya timu hiyo kutangaza kuachana na kocha Jose Mourinho hapo jana.
Katika post hiyo Paul Pogba aliandika “ Caption this “ na akaifuta baada ya dakika 10.
Mabosi wa Man United wamekasirishwa na post hiyo ya mchezaji huyo ikitazamwa kama ni ukosefu wa heshima.
Paul Pogba na Jose Mourinho hawakuwa na mahusiano mazuri tangu kuanza kwa msimu huu.