Messi akabidhiwa kiatu chake cha dhahabu
European Golden Shoe ni tuzo ambayo hupewa mchezaji ambaye ameongoza kwa kufunga magoli katika ligi kwenye ligi kubwa barani Ulaya.
Msimu uliopita 2017/18 Lionel Messi ndio alishinda tuzo hiyo kwa kufunga magoli 34 katika La Liga na kuwa mchezaji mwenye goli nyingi katika ligi kubwa Ulaya, Mo Salah wa Liverpool alishika namba mbili akifunga goli 32 kwenye ligi.
Jijini Barcelona leo Lionel Messi amekabidhiwa tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu ambapo ni mara ya tano kuchukua.
Hakuna mchezaji mwingine ambaye amechukua tuzo hiyo mara 5, Cristiano Ronaldo anashika namba mbili kwa kuchukua mara 4.
Misimu ambayo Lionel Messi amechukua tuzo hiyo
2009/10 — Magoli 34
2011/12 — Magoli 50
2012/13 — Magoli 46
2016/17 — Magoli 37
2017/18 — Magoli 34